Cherehani agawa vifaa vya michezo vijiji 112, Cherehani Cup 2025/30

Mbunge wa Ushetu mkoani Shinyanga, Emmanuel Cherehani amegawa vifaa vya michezo katika vijiji 112 jimboni mwake jezi na mipira,hatua hiyo ni maandalizi ya mashindano ya Cherehani Cup katika muhula wake wa pili wa ubunge 2025-2030.

Ugawaji huo unatekeleza ilani ya uchaguzi wa mwaka 2025 katika sekta ya michezo, huku lengo likiwa ni kuwajengea vijana fursa ya kukuza Vipaji na Ajira.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa vifaa hivyo Cherehani amesema mashindano ya Cherehani Cup yataanza ngazi ya vijiji kusaka mabingwa wa kata, Ambao ndiyo watakaoshiriki ligi ya jimbo inayo shirikisha maabingwa wa kata zote 20.

Aidha, amewahimiza Madiwani kuendelea kuweka hamasa ya uanzishwaji wa timu za mpira wa pete ili kundi la mabinti nalo liweze kunufaika na michezo.

Katika hatua nyingine, Cherehani ameahidi kuendelea kuwasaidia vijana wanaoibuka na vipaji kupitia mashindano hayo hadi kufika ngazi za wilaya, mkoa na Taifa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

0FansLike
0FollowersFollow
0FollowersFollow
0FollowersFollow
0FollowersFollow
0SubscribersSubscribe

Advertisement

spot_imgspot_imgspot_imgspot_img

Latest Articles