CHADEMA yatangaza Kamati Rasimu Katiba Mpya

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeitaka Serikali kutenga bajeti maalumu kwa ajili ya maandalizi ya uandishi wa Katiba Mpya, huku kikitangaza kuunda kamati ya watu 11 itakayoratibu uandaaji wa rasimu ya katiba pamoja na sheria itakayosimamia mchakato huo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya CHADEMA leo, Juni 17, 2026, Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, amesema wajumbe wa kamati hiyo watafanya kazi kwa kujitolea, huku baadhi ya shughuli zake zikitarajiwa kugharamiwa kupitia michango ya wananchi inayojulikana kama “Tone Tone”.

Mnyika amesema hatua hiyo inalenga kuharakisha maandalizi ya mchakato wa Katiba Mpya na kuonyesha dhamira ya chama katika kushirikisha wadau mbalimbali bila kutegemea fedha nyingi za umma.

Amebainisha kuwa tofauti na mchakato wa mwaka 2011 ulioongozwa na Tume ya Katiba chini ya Jaji Joseph Warioba, ambao uligharimu takribani Shilingi bilioni 120, kamati ya sasa itafanya kazi kwa mfumo wa kujitolea na kutumia rasilimali chache.

Kwa mujibu wa Mnyika, kamati hiyo itaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Dk. Rugemeleza Nshala. Katibu wa kamati atakuwa Wakili Deogratius Mahinyila, huku wajumbe wengine wakiwa Wakili Ali Ibrahim, Suzan Lyimo, Ruth Mollel, Wakili Gaston Garubindi, Pamela Massey, Zeudi Mvano na Boniface Jacob.

Aidha, mawakili Mpale Mpoki na Jeremiah Mtobesya, ambao si wanachama wa CHADEMA, watashiriki kama washauri wa kamati hiyo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

0FansLike
0FollowersFollow
0FollowersFollow
0FollowersFollow
0FollowersFollow
0SubscribersSubscribe

Advertisement

spot_imgspot_imgspot_imgspot_img

Latest Articles